Ads

DIWANI MTARAWANJE ,ATOA SOMO ZITO KWA WANAFUNZI WANAOSOMA SHULE ZA KATA.


Mwambawahabari 
Diwani kata ya kijichi jijini Dar es salaam leo ametembelea shule ya Sekondari  Mbagala  kuu iliyopo katika kata hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza shuleni hapo Diwani Mtarawanje amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii sambamba na kutokuwa na nidhamu mbaya kwa walimu.

Diwani Mtarawanje akiwa katika Picha ya Pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbagala  Kuu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Diwani)

Mtarawanje amewaasa wanafunzi hao kutokuwa watoro na pia kujiepusha katika suala zima la matumizi ya Dawa za kulevya kama vile Bangi,cokei, mirungi n.k.

Mwalim Mkuu wa Shule hiyo DEOGRATIUS MICHAEL NDILIME, akiongea na wanafunzi (Hawapo pichani) katika ziara ya  Diwani wa Kata ya Kijichi,Mh Eliasa  Mtarawanje.(kusoto) ni Mkamu Mwalimu Mkuu Bi.MARIAM KILONGO (Picha na Ofisi ya Diwani). 

Mh Diwani ametoa historia yake fupi ya maisha yake hasa ya kimasomo,amewaambia kuwa hata yeye alipitia katika shule za kata, hivyo ni jitihada pekee ambazo zimemuwesha kufikia malengo yake.

Diwani wa Kata ya Kijichini  Eliasa Mtarawanje akizungumza na wanafunzi ,leo katika ziara yake hiyo.

"Hata mimi nimesoma katika shule za kata ,kwa kipindi kile misingi ya elimu haikuwa bora sana kama kipindi chenu hivyo ni jitihada zangu katika kusoma,kwani sikuthubutu kupoteza muda katika mambo ya hanasa na hatimae nimeweza kufikia malengo yangu na hata nyinyi jitahidini kuishi kwenye ndoto zenu ambazo nzuri ili muje kutimiza malengo yenu''. Amesema Mtarawanje. 


Wanafunzi wa Sekondari ya Mbagala Kuu wakimsikiliza Diwani mtarawanje Akihutubia ,leo katika ziara yake shuleni hapo.

Mh Diwani Mtarawanje amesema atahakikisha kwa nafasi yake kupunguza baadhi ya changamoto katika shule hiyo ikiwamo kuongeza madarasa ,vyoo,vifaa vya michezo, samba na kupunguza changamoto zingine zinazowakabili walimu,ambapo amewataka waendelee kuongeza juhudi katika kuwaelimisha watoto hao.


Mh Diwani amesema yupo kwenye mpango wa kuanzisha Makongamano mbalimbali ya kuhamasisha vijana ,ikiwamo makongamano ya "Kijana Shtuka","Edu Talent"ambapo hii yote ni katika kuhamasisha vijana wanatengeneza mazingira ya kusoma kwa bidii lakini pia kupata wakati wa kukuza vipaji vyao.

No comments