Ads

MGOMBEA UBUNGE KINONDONI KWA TIKETI YA CUF ATOA AHADI HIZI

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi CUF Rajab Juma, ameeleza vipaumbele vinne ambavyo atavisimamia atakapopewa  ridhaa ya kiti hicho.

Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CUF Abdul Kambaya akimnadi Mgombea wa jimbo la Kinondoni Rajab Juma jijini Dar es Salaam.

Akiomba kura kwa wakazi wa Kijitonyama katika viwanja vya Alimaua  jijini Dar es Salaam, Juma alitaja vipaumbele hivyo kuwa ni elimu, afya, ajira na miundombinu.

“Kipaumbele cha kwanza ni elimu na nitakachofanya katika elimu utakapoletwa mswada wa elimu nitachangia hoja kutaka serikali iongeze mishahara kwa walimu ili wajikite zaidi katika kufundisha wanafunzi badala ya kufanya biashara ya kuuza biskuti shuleni, hii itaongeza ufaulu kwa wanafunzi,” alisema.

Afya, alisema baada ya mtu kuwa na elimu anatakiwa kuwa na afya, hivyo atahakikisha kunakuwa na mfuko maalum wa matibabu ambao utawaanezi wazazi wajawazito, watoto wachanga na wazee ili kupata matibabu kwa gharama nafuu.

Ajira, alisema akichaguliwa atasimama imara katika kuanzisha na kusimamia miradi midogomidogo ya wafanyabiashara wadogo kama vile bodaboda na kuwaunganisha kuweza kusajili katika vikundi ili wajitafutie riziki za haralina kwa ajili ya kujikimu kimaisha, kusaidia wazazi na kusomesha watoto.


Miundombinu, alisema maeneo mengi ya Kinondoni yameathirika kijografia na hayako salama pale mvua zinaponyesha kwani kila mahali panakuwa pamefurika maji hivyo atahakikisha miundombinu kama ya barabara inaboreshwa.

No comments