Ads

KAMATI YA SIASA YA CCM UBUNGO YA ANZA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI UBUNGO.

Kamati  ya Siasa ya chama  Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ubungo ziarani kukagua miradi ya maendeleo wilayani Ubungo,picha zote na John Luhende.

Mwambawahabari 
Kamati ya ya Siasa ya chama cha Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ubungo leo imeanza ziara ya siku mbili kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.
Akizungumza wakati akitoa maelezo mfupi kabla ya kuanza kwa ziara hiyo Mwenyekiti  wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja , amesema ziara hii ni utekelezaji wa  Ilan ya CCM ukurasa wa  229 na 230 Katiba Ibara   ya 76.

Aidha amewataka viongozi wa Wilaya hiyo kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo nakutojisikia usumbufu kutoa majibu kwa kila Watakayo ulizwa na Kamati hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Lipes Kayombo ameambatana Kamati hiyo kuwa yeye pamoja na watendaji wenzake wameahidi kutoa ushirikiano na maelezo ya kina kwa kila mradi ulio katika Wilaya hiyo. 

No comments