Ads

JAFO, MARUFUKU WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI KUFUNDISHA SHULE BINAFSI


Mbeya.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amepiga marufuku walimu wa shule za sekondari za serikali kufundisha vipindi katika shule binasfi nchini na kuagiza maofisa elimu kufuatilia.

 Waziri Sulemani Jafo 

Ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Ilomba katika halmashauri ya jiji la Mbeya.

Amesema walimu kufundisha vipindi shule binafsi ni changamoto inayochangia mdondoko wa elimu na kwamba mwalimu atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwamo kufukuzwa kazi.

"Serikali ya awamu ya tano imeboresha mazingira mazuri katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwalipa malimbikizo ya fedha zao sasa kitendo cha kukimbilia vipindi shule binafsi ni ukiukwaji wa kimaadili katika utumishi wa umma," amesema.

Pia ameagiza maofisa elimu sekondari kufuatilia mienendo ya walimu na kushirikiana na wazazi katika kufuatilia maadili ya wanafunzi wa kike ili kupunguza tatizo la mimba shuleni.

"Kuna mkoa mmoja ni aibu wanafunzi wa kike zaidi ya 100 wameacha masomo kwa ajili ya mimba sasa katika mkoa wa Mbeya hilo sijalipata nadhani ni kwa sababu ya utendaji mzuri wa mkuu wa mkoa na usisite kuwawajibisha wazazi wazembe," amesema.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema zaidi ya wanafunzi 3,000 hawakufanikiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018 kutokana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa 33.

"Waziri tunakuhakakikishi ifikapo Januari 26 vyumba vya madarasa vitakuwa vimekamilika na watoto ambao walikosa nafasi kuanza, wataanza masomo na huo ndio mkakati wangu wa mkoa kwa kushirikaina na wananchi na wadau wa elimu," amesema.


Ofisa elimu sekondari wa jiji hilo, Abuu John amesema katika shule ya Sekondari Ilomba wanafunzi waliochangulia kujiunga kidato cha kwanza ni 400 kati ya hao 157 walikosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

No comments