Ads

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA

Mwambawahabari

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuchagua viongozi bila kuangalia maslahi urafiki, dini, kabila kadhalika amewasihi kutochagua viongozi watoa rushwa kwa kusema kuwa rushwa ni adui wa haki

Amesema kiongozi anapaswa kuwa mfano kwa wanachama na wananchi. Hapaswi kutuhumiwa kwa sifa mbaya kama ujambazi, madawa ya kulevya, rushwa n.k. Kuna msemo maarufu unasema 'mke wa Mfalme hapaswi kutuhumiwa kwa kuchepuka'

"Sio siri kwa mageuzi tuliyoyafanya ni makubwa sana na hatuna budi kuyasimamia na viongozi waliochaguliwa ndio watakakuwa na majukumu hayo"  Alisema  Rais Magufuli
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk.John Magufuli akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi wakati akifungua kifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18, 2017.

No comments