Ads

KUMBILAMOTO "SIHUSIKI NA UBOVU WA BARABARA MUULIZENI JAFO NA " AFAFANUA KUHUSU TARURA, ASEMA ATASAMBAZA WARAKA WANANCHI WA KATA YAKE WAUSOME,AELEZA ALIVYOTIMIZA AHADI ZAKE.

Mwambawahabari
Katika kusherekea kutimiza miaka miwili ya kiutendaji tangia achaguliwe kuwa Diwani wa kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, amefunguka mazito ikiwa ni njia ya kwajibu wale wanaomrushia lawama  kuhusiana na utendaji wake wa kazi hususani kero ya Bara bara.
Akizungumza na wananchi wa  Kata ya Vingunguti CCM kwa Kombo Jijini Dar es Salaam katika kutimiza miaka miwili ya kiutendaji  , Diwani Kumbilamoto ambaye pia ni Naibu Meya bwa Manispaa ya Ilala, amesema kuingia kwake kwenye siasa ni kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi wanyonge waliompa heshima ya kushika kiti hicho na sio kwa ajili ya kupiga dili ya kuwa nyonya waliomchagua .
Aidha, Kumbilamoto, ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Wilaya ya Ilala, amewataka  wale wanasiasa wanaomchafua na kutaka kukuwagombanisha na Wananchi  wake waache mara moja kwani siasa hizo zinadidimiza maendeleo.
Kumbilamoto, amefanya  mkutano huo ikiwa ni  njia ya  kujitathimini  utendaji wake wa kazi na nguvu za usimamizi wa ilani ya Chama chake kilichompa ridhaa ya kuwa Diwani katika kipindi cha miaka miwili, kujua dhamira ya Wana Vingunguti  na kuona ni wapi walipotoka, walipo na wapi wanatakiwa kwenda.
"Ili nchi iwe na maendeleo ni lazima viongozi waepuke kufanyakazi kwa mazoea na kuweka siasa pembeni huku dhamira yao kuu ni kuweka vitendo mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo, kama tutakuwa na siasa nyingi za kuahidi au kupakazana matope maendeleo tunayoyataka tutayasikia kwa wenzetu, nchi bado sana tupo nyuma tunatakiwa kupambana na kutumia ubunifu wetu kusonga mbele".Amesema Kumbilamoto
Moja ya matatizo ambayo Diwani Kumbi lamoto amekuwa akilalamikiwa ni pamoja na suala la uchakavu wa miundombinu ya Bara bara ya Mnyamani na Vingunguti, jamabo ambalo amesema halimuhusu kwamba bara bara zote zipo chini ya Serikali kuu kupitia kwa TARURA zikisimamiwa na Waziri wa Tamisemi Suleimani Jaffo.
Katika changamoto hiyo, Diwani huyo amedai amekuwa akipokea vitisho na matusi hadi kufikia kutukanwa mzazi wake kuhusiana na ubovu wa Bara bara jambo ambalo  limekuwa likimuuma sana na ameamua kulitolea ufumbuzi ili kuepukana na maswali hayo yanayohusiasha mgongano wa kisiasa dhidi ya Chama chake cha CUF.
Hata hivyo, Kumbilamoto, amesema kuwa TARURA iliaznishwa kwa mujibu wa kisheria  kwamba ni chombo pekee kitakacho simamia miundombinu ya Bara bara kuanzia ngazi za Vijini na Mjini ikiwa chini ya Serikali kuu ambapo walikusudia kuimarisha miundombinu pamoja na kufanya maendeleo endelevu ya bara bara.
Pia amsema kama yeye ingekuwa ni kikwazo cha kutokutengenezwa ka bara bara hiyo, basi angejiuzuru ila kwa vile haipo chini yake na hana jukumu hilo yeye kazi yake ni kufanya ufuatiliaji na usimamizi ataendelea kuwatumikia wananchi wake kwa kuwaaminisha kwa kile anachokifanya kwenye kata yake bila ubaguzi na kwa vitendo zaidi.
Amewashukuru baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto waishio katika kata yake kwa ushirikiano mzuri wa kuwahabarisha watumiaji wengine kuhusu  kero ya bara bara huku pongezi kubwa zikienda kwa Wananchi  wake kwa uvumilivu wa mambo na ahadi  ambazo ameziahidi na kufanyiwa kazi
"Nataka kuwaambia sitotishika na mtu, nipo radhi kufa lakini nitasema ukweli daima , Vingunguti siyo ya Kumbilamoto, ni ya wananchi  wote na maendeleo ya wana vingunguti ni ya wote, tupuuze wanasiasa wanaotaka kutugombanisha tufanye kazi, tumechoshwa  kula mlo mmoja kama kiboko tunahitaji milo mingi zaidi".Ameongeza Kumbilamoto
Amewaomba Sungungu kutumia busara katika malindo yao kwani kazi yao ni kuhakikisha ulinzi na usalama na sio kupeleka maneno kutoka kwa familia wakifanya hivyo watakuwa wagombanishi wakubwa na watatoka kinyume na maadili ya kazi zao.
Naye Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ilala, Bakari Shingo, amesema maendelo ya Taifa huletwa na utendaji bora wa kazi, hivyo amewataka Viongozi kuacha kupiga domo badala yake wafanye kazi kwa Vitendo kama anavyofanya Kumbilamoto.

Mmmoja ya wakazi wa Vingunguti, Hadija Shabani, amesema kero ya Ushuru mkubwa wa ukusanyaji wa taka taka inayofika Shilingi 3000/= inawaumiza sana  huku kero hiyo ikionekana kuwa adha kwa wakazi wote waishio kata hiyo ambapo Mh: Diwani Kumbilamoto ameahidi kukaa na kamati yake kuangalia namna ya kutatua.
Miongoni mwa mafanikio ambayo yameonekana kuteka nyoyo za Wakazi wa Vingunguti ni pamoja na huduma za afya ambapo Zahanati ya Vingunguti haikuwa na Ambulence lakini kwa  sasa wamepatiwa, makusanyo ya juu ya pesa ya Zahanati kutoka Shilingi Milioni 2 kwa 3 hadi kufikia milioni 8-9 kwa mwezi, Mashine ya kufulia, Mashine ya presha na kisukari, tochi ya uchunguzi wa tonsi pamoja na kutanua Maabara ya Zahanati ya Vingunguti, kuboresha wodi za wazazi, kuwawekea TV Labour ambapo wazazi wamekuwa wakifuatilia  kinachoendelea duniani, kuongeza choo Zahanati ya Vingunguti ambapo awali kulikuwa na choo kimoja ila kwa sasa vipo viwili cha Madaktari na wauguzi pamoja na cha Wagonjwa, pamoja na kufunga Friji nne jambao ambalo lilitaka kupoteza hadhi ya Zahanati hiyo ambayo ilikuwa hatarini kufutwa kutokana na uchakavu wa miundombinu.
Katika upande wa Vijana , amefanikiwa kuimarisha mahusiano mazuri ya Vijana  kuwakutanisha pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha maisha yao kwa kuwakabidhi Boda boda kama kitega uchumi chao, kusaidia Jogging Klabu zilizopo Vingunguti na michezo kwa ujumla.


Diwani Kumbilamoto (kulia), akikabidhi Boda boda kwa Vijana wake ikiwa ni ahadi yake kwa mafanikio ya Wana Vingunguti. 
Upande wa Siasa amefanikiwa kutanua wigo mpana wa mawsiliano na kushirikiana na Serikali kuu ukizingatia ni Naibu Meya mwenye dhamana ya kusimamia maendeloa ya Ilala kwa kufuata kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Maendeleo hayana chama.
Shule ya Miembeni ilikuwa haina umeme ila kwa sasa ina umeme wa kutosha, kutoa vyerehani kwa wakina mama kama uanzishwaji wa Viwanda vidogo vidogo
,
 



No comments