WAZIRI MWAKYEMBE KUZINDUA MASHINDANO YA KANDA YA TATU YA KUOGELEA.
Mwambawahabari
Muogeleaji nyota wa kike wa Tanzania, Sonia Tumiotto.
Muogeleaji nyota wa Tanzania kwa upande wa wanaume, Collins Saliboko
……………..
Dar es Salaam. Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kesho Alhamis
atazindua mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika kwenye bwawa
la kuogelea la shule ya kimataifa ya Hopac.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Phillip Saliboko alisema jana kuwa
mashindano hayo yataanza saa 3.00 asubuhi na maandalizi yote
yamekamilika.
Saliboko alisema kuwa Waziri
Mwakyembe anatarajia kuwasili muda huo na mbali ya kuzindua, pia atawapa
hamasa wachezaji wa kuogelea wa Tanzania ambao watashiriki katika
mashindano hayo.
Saliboko alisema Tanzania
itawakilishwa na timu mbili, Tanzanite ambayo itakuwa na jumla ya
wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina la Platinum ambayo itakuwa
na wachezaji 21.
“Maandalizi yote yamekamilika na
wachezaji wamepata maandalizi Timu hizo zipo kambini hotel ya Giraffe
chini ya makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone, tuna
matumaini makubwa ya kufanya vyema,” alisema Saliboko.
Mmoja wa makocha wa timu hiyo,
Alexander Mwaipasi alisema kuwa wamemaliza mafunzo yao yote kwa
waogeleaji hao na wanatarajia kupata ushindi mkubwa.
“Kazi ya kufundisha tumemaliza,
iliyobaki sasa ni waogeleaji kufanya mambo yao kwenye bwawa, lengo ni
kutetea ubingwa, tupo tayari kwa mashindano,” alisema Mwaipasi.
Alisema kuwa timu yao inaundwa na
wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na wanaamini wataonyesha uwezo
wao na thamani yao ya kuwa katika timu ya Taifa.
“Nawapongeza sana wadhamini,
Giraffe Hotel, Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, Coca Cola, Label
Promotions , Print Galore na Slipway Hotel. Wametuwezesha kufanya
maandalizi makubwa katika mashindano haya, hatuta waaangusha,” alisema.
Mbali ya Tanzania, mashindano hayo
pia yatashirikisha waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Zambia, Afrika
Kusini, Sudan, Kenya na wenyeji Tanzania ambayo itawakilishwa na timu
mbili.
Wachezaji wanaoumda timu ya
Tanzanite ni Rania Karume , Chichi Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti
Gokarn, Sonia Tumiotto, Anjani Taylor ambao wote wanatoka klabu ya DSC,
huku wengine ni Natalie Abwooli Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff
(MSC), Sanne Kleinveld ( ISM Moshi), Angelica Spence, Tara Behnsen,
Tami Triller,Kayla Gouws na Amani Doggart ambao wanatoka klabu ya
Taliss.
Wachezaji wanaume ni Judah
Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O’Sullivan, Khaleed Ladha na
Matthew Guild wanatoka klabu ya Mwanza, Chris Fitzpatrick (ISM Moshi),
Marin DE Villard (DSC), Adil Bharmal, Hilal Hilal, Harry McIntosh,
Dhashrrad Magesvaran (Taliss) na wanaotoka klabu ya shule ya kimataifa
ya Morogoro ni Joseph Sumari, Collins Saliboko na Dennis Mhini.
Wachezaji wanaounda klabu ya
Platinum kwa upande wa wanawake ni Shivan Bhatt, Natalia (Taliss),
Charlotte Sanford, Vanessa Dickson (MIS), Rebecca Guild, Meredith Boo
(MSC), Maria Bachmann ( ISM Moshi), Kayla Temba na Maya Somaiya ambao
wote wanatoka klabu ya DSC.
Wanaounda timu ya wanaume ni
Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham
Kayugwa( ISM Moshi), Terry Tarimo, Aliasgar Chakera(Taliss), Zeke Boos
(MSC), Yuki Omari, Augustino Lucas (Champion Rise), Fallih Ahmed
(Taliss), Carter Helsby (MSC), Ian Lukaza(ISM) na Emmanuel Stenson wa
shule ya kimataifa ya Morogoro.
Post a Comment