Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kuzibadilisha kuwa mbolea kitakachojengwa na kampuni ya CRJE ya nchini China ambapo ujenzi huo unatarajia kuanza kesho.
Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio la kusaini mkatabahuo, Meya wa Manispaa hiyo ,Benjamini Sita amewaeleza kuwa kusainiwa kwa mkataba huo itasaidia kuweka maeneo ya manispaa hiyo kuwa safi ,na mbolea aina ya mboji itakayozalishwa na kampuni hiyo itakuwa rafiki kwa udongo na mazingira kwani haina kemikali .
Aidha , amesema kuwa kujengwa kwa kiwanda hicho kitaongeza ajira kwa wananchi pia kitawasaidia wakulima kutumia mbolea ambayo ni bora na ya kisasa huku ikiwa haina athari kwa udongo na hata mazao.
Pamoja na hayo sitta amaesema kuwa , kupitia mkataba huo manispaa ya Kinondoni itakuwa imeunga mkono kiasi kikubwa jitihada za Rais Magufuli katika kuelekea Tanzania ya viwanda, hivyo wananchi watapata ajira itakayo wasaidia kujikimu kimaisha .

Post a Comment