NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA UKANDA WA MTO NILE, ZAPEWA CHANGAMOTO KUFANYA UTAFITI WA KISAYANSI KUHUSU UCHAFU WA MAZINGIRA YA MTO.
Na John Luhende
mwambawahabari
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mh.Samia
Suluhu Hassan ametoa changamoto kwa Jumuia ya Ukanda wa Mto Nile kuhakikisha
unafanya utafiti ili kubaini sababu zinazochangia kuwepo kwa uchafuzi wa
mazingira ndani ya Mto huo.
Mh.Hassan ameyasema hayo leo wakati akihotubia nchi
wanachama wa Jumuia hiyo kwenye maadhmisho ya sherehe ya Siku ya Mto
Nile,ambapo kwa mwaka huu yamefanyika Nchini Tanzania, nakusema kuwa Mto huo
unasaidia mambo mbalimbali yakiuchumi ikiwemo Umeme,Uzalshaj wa Chakula pamoja
na kupatikana kwa maji yanayotumika kwa shughuli zingine kama vile majumbani.
Nchi ambazo zinaunda Jumuia hiyo ni zile ambazo zimepitiwa
na Mto Nile ambapo ni
Tanzania,Uganda,Kenya,Ethiopia,Burundi,Rwanda,Dr.Congo,Misri,Sudani
Kusni,Sudani,ambapo wawakilishi wan chi hizo wamepata fursa yakujadili namna ya
kuboresha hali ya mazingira katika Mto huo.
Kwa upande wakeWaziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gryeisoni Lwenge amesema kuwa
Tanzania imepiga hatua kwa asilimia 72 kwa wananchi wake wanaoish maeneo ya
vijjini kupata huduma za maji safi na salama huku akidai kuwa nchi zingine za
jumuiya hiyo zina asimia chni ya 50 nakwamba zimekuwa zikija Tanzania kujifunza
namna yakuboresha miundombnu ya maji.
Amesema kuwa kwa sasa
changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza ni pamoja na nchi nne kati ya
kumi ambazo ni wanachama wa jumuiya hiyo
kushindwa kusaini mkataba wa mpito makubaliano ya kulinda mazingira ya Mto Nile
ambazo ni Misri,Sudani,Burundi,Congo,pamoja na kuchelewa kulipia ada ya umoja
huo.
Maadhmisho ya Siku ya Mto Nile kwa mwaka huu yamefanyika
kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam na kauli
mbiyu ikiwa ni Mto wetu Chanzo cha Nishati,Chakula,na Maji kwa Wote.
Post a Comment