ASILIMIA 61 YA WANAFUNZI WANAOMALIZA ELIMU YA JUU KATIKA VYUO MBALIMBALI NCHINI HAWANA UJUZI NA SIFA ZA KUAJIRIWA
Na Jesca Mathew
mwambawahabari
Asilimia 61 ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini hawana ujuzi na sifa za kuajiriwa kweny sekta binafsi ili kukuza uchumi na kufikia kiwango cha kati .
Hayo yamebainishwa leo na Naibu waziri wa kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde wakati akizungumza na wadau wa makampuni ya sekta binafsi jijin Dar es salaam na kusema kuwa baada ya kugundua changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wameanzisha mpango wa miaka 5 wa kuwasaidia vijana kupata mafunzo kwa vitendo ili kuongeza sifa ya kuajiriwa na kujiajiri.
''Tumeamua kuanzisha programu hiyo ili kuhakikisha wanasaidia nguvu kazi ya nchi kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri lakini pia kuajiriwa katika makampuni mbalimbali yenye uhitaji wa wafanyakazi walio bora katika utendaji kazi" alisema Mavunde.
Mheshimiwa mavunde akaongeza kuwa programu hiyo ya miaka 5 iliyoanza mwaka 2016 na kutegewa kumalizika na kufikia mwaka 2021 unatarajiwa kuwafikia watu milioni 4 ili kuwasaidia kukuza ujuzi na kufikia uchumi wa kati kwa kuwepo nguvu kazi ya juu ya asilimia 34.
''Mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana elfu 2000 ambapo wamepata nafasi ya kujiunga katika mafunzo na kupata ujuzi katika kiwanda vya nguo EPZA pamoja na vijana elfu 1000 kupata mafunzo ya kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi katika mikoa mbalimbali ikiwemo morogoro .'' Aliongeza Mheshimiwa Mavunde.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa sekta binafsi Tpsf ameeleza kuwa sababu za kukosa ujuzi ni sababu kubwa inayosababisha waajiri kuajiri watu kutoka nchi za nje kutokana na wazawa kukosa viwango vya utendaji kazi.
''Kuna haja ya kuwepo kwa mafunzo yatakayosaidia kuwapa ujuzi wa kufanya kazi pindi wanapoajiriwa japokuwa tatizo hili haliko tanzania pekee hata kea nchi jirani kama kenya.''alieleza simbeye.
Hata hivyo MKurugenzi huyo amewataka waajiri wa sekta binafsi kutoa kipaumbele za ajira kwa vijana wa kitanzania ili kuendelea kuunga mkono kazi inayofanywa na serikali kwa kuwa inatumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo.
Post a Comment