RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA CHAD NA MWENYEKITI MPYA WA KAMISHENI OJA WA AFRICA
mwambawahabari
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20 Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu yake jijini N'Djamena, Chad. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Chad Mhe. Ahmat Ghazali Acyl na Waziri wa Fedha Mhe. Diguimbaye Christian.
Ziara hiyo ya Rais Mstaafu nchini Chad ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Deby wamezungumzia janga kubwa linaloinyemelea dunia na hasa nchi za uchumi wa kati na chini ikiwa hakutafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu. Viongozi hao wamezungumzia haja ya nchi za bara la Afrika kuchukua hatua z amakusudi kufanya maboresho na mageuzi makubwa katika sekta ya elimu katika nchi zao ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea. Azma hiyo inatokana na stadi kuwa nchi za uchumi wa kati na chini zko nyuma kielimu kwa miaka 50 hadi 70. Aidha, lipo tishio kuwa ifikapo mwaka 2050, kazi na ajira takribani bilioni 2 zitakuwa zimefutwa kutokana na maendeleo na matumizi ya teknolojia (automation).
Rais Deby amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Mbali na mkutano wake na Rais wa Chad, Rais Mstaafu amekutana pia na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika (AU) na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe. Moussa Fakhi nyumbani kwake N'Djamena. Rais Mstaafu amempongeza Mhe. Fakhi kwa kuchaguliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya. Viongozi hao wawili wamekuwa pia na mazungumzo yaliyohusu mipango ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu barani Afrika na masuala ya hali ya usalama ya Libya.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo jijini N'Djamena, Chad.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo jijini N'Djamena, Chad.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena.
Post a Comment