TANZIA ,BODI YA FILAMU TANZANIA INATANGAZA MSIBA WA MWIGIZAJI NGULI MAREHEMU HAJJI JUMBE
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BODI YA FILAMU TANZANIA
Bodi ya Filamu Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mwigizaji Nguli Marehemu Hajji Jumbe kilichotokea tarehe 24/10/2016 katika hospitali ya kwa Dkt. Mvungi, Kindondoni, Dar es Salaam.
Marehemu Hajji Jumbe ni miongoni mwa waigizaji nguli ambaye mchango wake utaendelea kukumbukwa sana. Marehemu ni kati ya waigizaji walio na wafuasi wengi na aliyetokea kupendwa sana na mashabiki wa filamu na maigizo. Kwa siku za karibuni, Marehemu ameongeza idadi ya wapenzi na mashabiki wake kupitia Tamthiliya ya Siri za Familia inayoendelea kurushwa katika kituo cha televisheni cha EATV.
Kazi zingine alizozifanya ni pamoja na Filamu ya Siri ya Mama, Kelele, Kaone Jiwe na nyingine nyingi.
Marehemu hajji Jumbe alianza kazi ya Uigizaji na Filamu mwaka 2005 hadi mauti yalipomkuta.
Bodi ya Filamu Tanzania, Wanatasnia ya Filamu, Waigizaji na Wadau wote tumeguswa sana na msiba huu wa mpendwa wetu Marehemu Hajji Jumbe. Katika kuuenzi umahiri na unguli wake kupitia kazi zake hatuna budi kuendeleza yale yote aliyochangia katika kukuza na kuendeleza Sekta ya Filamu na Uigizaji Nchini.
Bodi inatoa pole kwa wote walioguswa na msaiba huu. Pole za pekee ziwaendee Familia yake Mke na Watoto, Ndugu wa Marehemu, Shirikisho la Filamu, Chama cha Waigizaji, Wanafamilia wa familia ya Tamthiliya ya Siri za Familia, Wanatasnia ya Filamu, wapenzi wa filamu na wadau wote kwa kuondokewa na Mpenndwa wetu Hajji Jumbe.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
IMETOLEWA NA KATIBU MTENDAJI WA BODI YA FILA

Post a Comment