WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAHAMASISHWA KUNYWA DA ZA KUZUIA MABUSHA ,USUBI NA MATENDE
Na;Rayusa Yasini
mwambawahabari
WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam wameombwa kuchangamkia fursa ya zoezi la Unywaji dawa za magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kwa jamii ili waweze kujikinga na magonjwa hayo.
Magonjwa hayo ni pamoja Mabusha, matende, usubi, Minyoo zitakazo kuwa zinatolewa katika vituo vya afya vyote vya mkoa pamoja na kwenye mikusanyiko ya watu.
Akizungumza leo katika uzinduzi wa zoezi hilo la unywaji wa dawa hizo litakalochukua siku tano mganga mkuu wa mkoa Grace Magembe amesema wagonjwa watakaopatikana na tatizo hilo la watafanyiwa upasuaji.
“Tumeandaa vituo vya afya pugu, na Mbweni mission ambako upasuaji utakuwa unaendelea huku tukishirikiana na madaktari kutoka hospitali ya Muhimbili.”
Ameongeza kuwa mpaka sasa zoezi la upasuaji litaendelea hadi mwezi wa 12 mwaka huu, ambapo mpaka hivi sasa zaidi ya wagonjwa 104 wameshafanyiwa upasuaji.
“Zoezi hili tumelipa sana kipaumbele ili kuokoa nguvu kazi ya taifa, tumeandaa vituo zaidi ya 281 kwa ajili ya zoezi hili wanaume kwa wanawake wajitokeze kumeza dawa hizi”.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi kuepuka maneno yayozungumzwa mitaani kuwa dawa zinamadhara hivo kujitokeza kumeza dawa ili waepukanae na magonjwa hayo.
“Zoezi linaendelea vyema watanzania wajitokeze, pia na zoezi la usafi liendelee ili kuepuka mazalia ya mbu ambao ni vigumu kuwatambua wanaeneza ugonjwa huu’’.
Wizara ya afya na ustawi wa jamii ilianzakuendesha zoezi hili kuanzia mwaka 2009, wananchi zaidi ya milion 4 wanatarajiwa kufikiwa na huduma hiyo katika jiji la Dar es salaam.
Post a Comment