SHIVYAWATA YAITAKA WIZARA YA AFYA KUWATAMBUA WATU WENYE ULEMAVU NA KUWAPA HAKI YA MATIBABU
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya watu wenye ulemavu nchini (SHIVYAWATA) Ummy Nderinanga pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho hilo wamemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu kujua na kuwatambua watu wenye ulemavu hapa nchini katika kupata haki ya msingi ya huduma za Afya Mahospitalini na sehemu zingine za huduma hiyo.
Hayo yamejiri leo Jijini Dar es Salaam,wakati akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti huyo wa SHIVYAWATA, akirejea kauli iliyotolewa amesema hivi karibuni na Waziri wa Afya iliyotangwa na vyombo vya Habari akisisitiza makundi matatu yanayopaswa kupatiwa huduma za Afya bila malipo kuwa ni Watoto , Wazeee na wamama wajawazito huku akiwasau kundi la watu wenye ulemavu
Bi.Ummy amesema wanaiomba wizara husika kufanya maboresho ya waraka Wa mwaka 2012 ili huduma na tiba Vila malipo kwa watu wenye ulemavu isiishie kwenye hospital, zahanati tu Bali hata katika hospitali za rufaa.
"Hali hii imetusikitisha sana SHIVYAWATA na huenda ikaleta athari kubwa kwani haiendani na Sera ya Afya ya Taifa na Waraka wa Serikali uliosema ambapo watu wenye ulemavu wapatiwe huduma bila malipo katika Hospitali, Zahanati na vituo vya Afya vya Serikali" amesema
Aidha wameiomba serikali kuwapatia bima za Afya watu wenye ulemavu ili kuepuka udhalilishaji na urasimu katika kupata msamaha wa malipo wa huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma.
“huduma hii iwe katika huduma na dawa zote katika hospital zote na maduka binafsi ya dawa yatakayopendekezwa na itambue vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ikiwemo viti mwendo, fimbo myeupe" amesema
Hata hivyo Ummy aliongeza kuwa, wanapinga hatua ya utambulisho wao wa kupatiwa huduma ambapo vielelezo vyao wanapoviwakilisha katika ‘DIRISHA LA MAMA HURUMA’ neno hilo wanalipinga kwa kuwa huduma ya afya ni haki yao na sio huruma" amesema
Mwenyekiti wa chama cha walemavu wasiosikia Habibu Mrope ameiomba serikali kuwasaidia kundi hilo kuwawekea vitambulisho vitakavyowatambulisha pindi wanapofika katika vituo vya Afya.
" utakuta tumepanga folen ya kusubiri majibu unaitwa hausikiii ila tukiwekewa utaratibu mzuri hii Changamoto hitakuwepo" amesema
Post a Comment