Ads

Watanzania waondolewa hofu ya kusoma nchini India

Na: Frank Shija,
mwambawahabariblog 
Watanzania wahasishwa kujiunga na masom katika Vyuo na taasisi za masomo zilizopo nchini India kwaku kuna fursa nyingi za kupata elimu na ni nchi salama kwa wageni waishio nchini humo.

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa EdCIL (India) Limited, Bw. Diptiman Das wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kusoma nchini India ijulikanayo kama Study in India Campaign iatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia tarehe 18 hadi 19 Februari.

Diptiman amesema kuwa kupitia Kampeni hiyo Watanzania watapata fursa ya kuunganishwa na Vyuo vikuu zaidi ya 712 vyuo vya kati  36671 na Taasisi zaidi ya 11445 zinazotoa taaluma katika fani za Uhandisi,Udaktari,Famasia, Nesi, Uongozi, IT, Bio-technology, Media Studies, Kilimo na Hotel Management


Kwa upande wake Balozi mdogo wa India hapa nchini Robert Shetkintong amesema kuwa India imekuwa ikisaidia Serikali ya Tanzania katika mafunzo mafupi kwa watumishi wa umma ambapo kila mwaka karibu wafanyakazi 300 wa Serikali upelekwa India kwa ajili ya mafunzo mafupi.

Aidha Balozi huyo amewatoa hofu Watanzania kuwa India ni mahali salama kwa kusoma pamoja na changamoto zilizojitokeza za baadhiwanadunzi wa Kitanzania kupata usumbufu na kuongeza kuwa hali hiyo inawezakujitokeza sehemu yeyote na siyo jadi ya nchini mwao na kuwahakikishia Watanzania kuwa hali ya kiusalama ni shwari.

EdCIL ni Taasisi inayojiendesha kwa faida imesajiliwa kwa na kupata cheti  cha Serikali ya IndiaISO 9001-2008 & 14001 : 2004 kupata cheti  cha Serikali ya India,chini ya Wizara ya Maendeleo ya Rasilimali Watu ya Serikali ya India.Taasisi hii inatumika kuitangaza Elimu ya India kimataifa na kuwadahili wanafunzi katika vyuo na taasisi zilizopo India.



No comments