Dkt Kigwangalla autaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kurekebisha mapungufu yaliyopo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alisamiliana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu mara baada ya kuwasili mkoani humo jana jioni kwa ajili ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia mfumo wa makusanyao ya mapato kwa kutumia mtandao, ambao unafanya kazi sehemu ya usajili tu(mapokezi) kutokana na hali hiyo liagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha unagunga mtandao huo kwenye maeneo yote ya malipo ili kuhakikisha mapato hayapotei.Aliyekaa katika kompyuta ni Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Asteria Mbele na kulia ni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt Rita Lyiyamuya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia jana baadhi ya vifaa vya maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia na kuhoji ni sababua zipi zinazosababisha mashine ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ,figo na ini (BIOCHEMIST) ambayo haifanyi kazi mara baada ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .Kushoto Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimwaagiza kuhakikisha taa za vyumba vya upasuaji zinafanya kazi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu ambapo alitoa muda wa siku 60 wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .Pia alitoa muda wa miezi sita wa kufanya marekebisho ya baadhi ya majengo.
Post a Comment