Ads

TAN GREEN WASAIDIA MITI 500 KATIKA SHULE YA MSINGI BUNJU.

TAN GREEN WASAIDIA MITI 500 KATIKA SHULE YA MSINGI BUNJU.
mwambawahabariblog
Taasisi ya kijamii la Tan Green ambayo inajishughulisha na kupambana na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa kwa kutoa elimu na kupanda miti leo imetoa msaada wa miche ya miti 500 katika shule ya msingi Bunju iliyopo bunju wilaya ya kinondoni jiji dar es salaam katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Zoezi la kusaidia kutoa miche hiyo ya miti limefanyika mbele ya mbunge wa Maswa Mashariki ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya mazingira bungeni Stanslaus Haruni Nyongo huku likipewa Baraka na baadhi ya viongozi wa taasis ya Turn green na viongozi wengine ndani ya kata ya Bunju.
IMG-20160212-WA0010
Mh. Stanslaus Nyongo Mbunge wa maswa mashariki akipanda mti katia shul e ya msingi Bunju.
Mh. Nyongo ameitaka jamii itambue kuwa athari ya uharibifu wamazingira ni tatizo aambalo linamkumba kila mmoja hivyo jamii ishiriki kikamilifu katika kupambana na aina yoyote ya uharibifu wa mazingira, na itambue umuhimu wa kuwa na mazingira salama,
Pia ameitaka serikali kuweka mkazo wa matumizi mengine ya nishati ukiachilia mbali matumizi ya mkaa katika baadhi ya mikoa ambayo hiko hatarini kuingia katika hali ya ujangwa, “kuna baadhi ya mikoa inaelekea kuwa ni jangwa kama serikali haitatafuta mbadala wa matumizi ya nishati ya mkaa, na ningependelea mikoa hiyo ipewe kipaumbele cha matumizi ya nishati nyingine kama gesi”, alisema
IMG-20160212-WA0006
Naye kiongozi wa taasis hiyo Martha Nghambi ameizitaka taasis na jamii ya kitanzania kushirikiana katika kupambana na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa, huku akizitaka taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuchukulia tatizo hilo ni letu sote na kutoa dhana ya kushindana kwani wote wana nia na dhumuni moja.
IMG-20160212-WA0005
Kwa upande wake mwalimu Ezekiel Joseph Nichombe mkuu katika shule hiyo ameishukuru sana shirika  hilo kwa msaada wa miti hiyo na kuhaidi kusimamia ipasavyo na kutoa rai ya kushiriki katika mashindano ambayo yatafanywa na shirika hilo lenye kushindanisha shule kadhaa katika kutunza mazingira.

No comments