MAUZO SOKO LA HISA LA DAR ES SLAAM ( DSE) YAPANDA
Mauzo ya soko
Idadi ya mauzo imeongezeka zaidi ya mara 4 hadi Bilioni 54.4 kutoka Bilioni 11.3.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepanda zaidi ya mara 2 hadi Milioni 35.1 kutoka Milioni 13.1.
Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1. NMB kwa asilimia 62.75%
2. CRDB kwa asilimia 36.86%
3. DCB kwa asilimia 0.15%
Idadi ya Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kutoka Trilioni 20.8 hadi Trilioni 21.1 wiki hii.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebakia kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 9.
Viashiria (Indeces)
· Kiashiria cha sekta ya viwanda kimepungua pointi 80.81 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta za TBL (1.67%), TCC (1.64%) na TOL (1.3%)
· Kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na za kifedha kimeshuka pointi 26.15 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta za NMB (1.86%) na DCB (0.9%).
· Kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara kimepanda kwa pointi 25.11 kikiwa kimechangiwa na ongezeko la bei ya hisa kwenye kaunta ya SWISSPORT (0.89%)
Post a Comment