CHAWATA YALIA NA SERIKALI KATAZO LA BAJAJI MJIN
Na John Luhende
mwambawahabariblog
CHAMA cha walemavu Tanzania(CHAWATA) kimeiomba Serikali kuondoa zuio la baadhi ya waendesha bajaji wenye ulemavu ambao sio wamiliki wa bajaji hizo,wasiingie katika usafirishaji huo wa haraka mjini.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana,Mwenyekiti wa chama cha walemavu Tanzania(CHAWATA) John Mlabu alisema kuwa omba omba wengi mjini wanaongezeka hasa walemavu kwakuwa wamekosa elimu ya kutosha,nakushindwa kuendesha maisha kwakuwa nawao wanamajukumu kama watu wengine.
Mlabu alisema kuwa wao kama walemavu ni vyema wakapewa nafasi ya upendeleo katika jamii kwa jambo ambalo wanaliweza kulifanya hasa katika kazi ya usafirishaji wa abiria kutumia bajaji katika katikati ya jiji.
Mwenyekiti Mlabu aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa walemavu katika serikali yake kwa lengo la kutetea na kuamini kuwa ni binadamu kama binadamu wengine wanaoweza kufanya kazi,hivyo ni vyema viongozi waandamizi wa serikali wafuate.
“kama walemavu wa usafirishaji wa baajaji wanatakiwa wamiliki mbona waendesha mabasi ya abiria na madereva taxi wao sio wamiliki na wanaruhusiwa kufanya kazi hizo “alihoji
Ametoa wito kwa madereva wa bajaji waliopata fursa ya kuendesha usafiri huo katikati ya jiji kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa kwa lengo la kuaminiwa.
Hata hivyo chama cha walemavu Tanzania(CHAWATA) kimetoa wito kwa serikali hasa Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam Kukaa meza moja na wadau kwa lengo la kuondoa unyanyasaji unaofanayika dhidi ya walemavu pamoja na kuondoa utegemezi walemavu Tanzania.
Mbali na hayo pia ametoa pongezi kwa Rais wa awamu ya tano Dkt.John Pombe Magufuli kwa kufanya uteuzi wa kuwateua Makatibu wakuu na Mawaziri bila ya kujali ulemavu wao ,hivyo basi “tunamuomba Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea hivyo na hata katika uteuzi wa wakuu wa mikoa kufanya hivyo”alisema
Post a Comment