Ads

TANZANIA YASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO MAKAMPUNI YANDANI KUJIENDESHA KIBIASHARA.

Meneja Biashara na Mauzo wa soko la hisa la Dar es salaam DSE Patrick Mususa 

mwambawahabariblog

Tanzania imeshauriwa kuwajengea uwezo wawekezaji wa ndani ili kuweza kujiendesha kibiashara kwa kuboresha miundo mbinu iliopo   ili kuweza kukuza uchumi na kuorodheshwa katika masoko ya hisa ya kimataifa.

 Wito huo umetolewa na Meneja Biashara na Mauzo wa soko la hisa la Dar es salaam DSE Patrick Mususa wakati akitoa taarifa za mwenendo wa soko la hisa la Dar es salaam ambapo amesema kuwa hatua ya makampuni kujiorodhesha katika masoko ya hisa ya nje ya nchi haina athari kiuchumi .

‘’Uwezo wa Tanzania kuendesha masoko ya hisa upo katika kujenga miundombinu yakiuchumi kwa kutiamkazo kwa wawekezaji wandani kuweza kujiendesha ‘’Alisema Meneja Mauzo na Bishara Patrick Mususa .

Mususa alisema kuwa mabadilko yaushindani wa makapuni kujiorodhesha katika masoko yahisa yakimataifa kunawezesha mabadiliko ya bei katika masoko yahisa yakimataifa .

Alisema kuwakatika makampuni ya  ndani yaliyo orodheshwa kimataifa nipamoja Acasher mining ambayo iliyorodheshwa katika masoko ya hisa yanchini Uingereza .

‘’Mchakato huu unawezesha makapuni ya ndani kuwa na ubia na makapuni ya nje ilkuweza kujiendesha kisoko nakuweza kujitangaza kimataifa ‘’Aliongeza Mususa .

No comments