MAJALIWA AKABIDHIWA NAKALA YAKE YA FOMU YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea nakala yake ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kutoka kwa Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambako ilitiwa saini na kamishina huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao walikwenda ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 15, 2016 kumpatia nakala yake ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti hiyo ambako ilitiwa saini na Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda (wapili kulia).Kushoto ni Katibu wa Idara ya Viongozi Watumishi wa Umma, Secretarieti ya Maadili , John Kaole na kulia ni Katibu wa Idara ya Viongozi wa Siasa, Secretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post a Comment