BODI YA MIKOPO HAKUKALIKI WAKURUGENZI WANNE WAPIGWA PIN; NDALICHAKO ASEMA MAOVU YAO HAYAVUMILIKI
mwambawahabariblog
Waziri wa Elimu
Sayansi, Tekinolojia na
ufundi Mh Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa mkurugenzi mtendaji
wa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa Rlimu ya juu,bw George R .Nyatega kuanzia leo, nakuwasimamisha
wakurugenzi wengine wanne wa bodi hiyo
kwa matuizi mabaya ya fedha ya bodi hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mh Ndalichako amewataja
wakurugenzi wengine kuwa ni ,bw Yusufu Kisare ,mkurugenzi wa fedha na utawala,
Juma Chagonja mkurugenzi wa urejeshaji mikopo ,Onesmo Laizer, mkurugenzi wa
upangaji na utoaji mikopo ,amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika
kuwa kulikuwa na udhaifumkubwa katika
utendaaji na kufanya malipo yasiyo
sahihi.
Aidha ameyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni kulipa mikopo wanafunzi zaidi ya marambli na
vyuo tofauti na wanafunzi wanao soma nje ya nchi kupewa mikopo miaka saba
badala ya miaka mine ,wanafunzi wasio na usajili kulipwa pesa katika vyuo
mbalimbali wanafunzi walio acha vyuo
kuendelea kupewa mikopo ,wanafunzi 143 kulipwa
mikopo miaka amayo hawakusajiliwa ambapo zaidi ya sh173,700 zililipwa
kinyume na utaratibu wana funzi 54,299
walipangiwa mikopo wakati hawakuomba.
Post a Comment