Makampuni jitokezeni kujitangaza kupitia uwanja wa Taifa
Na Lilian Lundo
mwambawahabariblog
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameyataka makampuni na wafanyabiashara
kutangaza biashara zao kupitia uwanja wa Taifa.
Mhe.
Majaliwa aliyasema hayo jana katika mkutano wa wadau wa michezo wakiwemo
wadhamini wa michezo, vyama vya michezo vya Taifa na
mashirikisho uliofanyika katika moja ya kumbi zilizopo uwanja wa Taifa.
“Uwanja
wetu una hadhi ya kimataifa lakini uwanja huu hautumiki kutangaza biashara
yoyote kama chanzo cha
mapato, badala yake kuta za uwanja zimezungukwa na giza hasa muda
cha usiku,” alisema Mhe. Majaliwa.
Mhe.
Majaliwa aliongeza kwa kusema kuwa kama
uwanja huo utazungukwa na mabango ya matangazo yataupandisha hadhi na kubadilisha mandhari ya uwanja hasa
muda wa usiku na fedha
zitakazopatikana zitatumika kuboresha uwanja huo.
Hivyo
Mhe. Majaliwa amewataka wadhamini wa michezo kujitokeza kwa wingi kutumia fursa
hiyo ya kutangaza bidhaa au huduma wanazozitoa kupitia uwanja wa Taifa ambao
hutumika katika mechi nyingi za kitaifa na kimataifa zinazochezwa nchini.
Aidha,
Mhe. Majaliwa amesema kuwa Tanzania itaendelea kupata heshima kupitia sekta ya
michezo kwani michezo ni kielelezo kinachoweza kutambulisha utamaduni wa Taifa
hivyo wadau wa michezo washikamane na Serikali na kuona ni namna gani matatizo
ya michezo yatatatuliwa na michezo kuendelezwa nchini.
Serikali
ya awamu ya tano imejipanga kuendeleza michezo nchini kwa kuweka misingi imara
ya kuendeleza michezo kuanzia umri wa chini, kurekebisha sera na sheria za
michezo ziliopitwa na wakati, kujali mafanikio, matatizo na mambo muhimu
yanayohusu michezo.
Post a Comment