WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KULIOMBEA TAIFA DHIDI YA JOTO KALI
Baadhi ya athari za kuongezeka kwa joto hupelekea kunyesha mvua kubwa na kusababisha mafuriko ,kama inavyoonekana pichani |
Na Beatrice Lyimo
mwambawahabariblog
Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi
ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kumuomba Mungu dhidi ya hali ya hewa ya
joto kali nchini.
Mwenyekiti wa Good News for All
Ministry, Askofu Charles Gadi akizungumza na waaandishi wa habari (Hawapo
pichani) kuhusu mkutano wa maombi siku ya Jumatano ya tarehe 20
Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki Feri ili kuomba Mungu kuepusha
ongezeko la joto nchini kushoto ni Katibu wa Good News For All Ministry
Mchungaji Palemo Massawe. Picha na Beatrice Lyimo
Askofu huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya Mamlaka ya hali ya hewa kuonyesha hali ya joto kufika nyuzi joto 35°C.
Askofu Gadi ameongeza kuwa, wanatarajia kufanya mkutano wa maombi siku
ya Jumatano ya tarehe 20 Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki
maarufu kama Feri ili kuomba Mungu kuepusha ongezeko la joto nchini.
“Joto limesambaa katika maeneo ya pwani hususani Dar es Salaam,
Tanga, na visiwa vya Zanzibar, hivyo kwa hali hii tumeona tufanye mkutano wa
maombi mafupi katika eneo la Soko la samaki la feri siku ya Jumatano kuanzia
saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana,
“Mungu amenipa nafasi ya kuomba dhidi ya majanga ya kimazingira
kama haya hivyo tunawakaribisha watu wote wa Dar es Salaam tuje tumlilie Mungu
kwa pamoja ili tuondokane na janga hili la joto na madhara ya Elnino”
alifafanua Askofu Gadi.
Kwa upande wake katibu wa Good News For All Ministry Mchungaji
Palemo Massawe amewataka Wananchi kuchukua hatua ili kujikinga dhidi
ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka.
Uongozi huo unaendelea na maombi ya kumuombea Rais John Pombe
Magufuli kufanikiwa katika juhudi zake za kulikomboa nchi kiuchumi na kielimu.
Post a Comment