Na Raymond Mushumbusi
mwambawahabariblog
Polisi mkoani Mwanza
imekanusha kuhusika na uhalifu kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya
habari hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Justus Kamugisha alipokuwa akizungumza ofisini kwake kuhusu tuhuma zilizotolewa
juu ya Jeshi la Polisi mkoani humo kuhusika na Uhalifu.
Kamanda Justus Kamugisha
amesema kuwa kuna taarifa zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyombo vya habari
kuwa Jeshi la polisi mkoani humo linajihusisha na masuala ya uhalifu ikiwemo
baadhi ya maofisa wao kushirikiana na wahalifu katika uuzaji wa dawa za kulevya
pamoja na kushirikiana na majambazi kupora mali za wananchi .
“Ni habari za uongo na
za kulichafua Jeshi la Polisi na mimi kama Kamanda wa Polisi nimelipokea suala
hili kwa masikitiko na natoa onyo kwa vyombo vya habari na jamii kwa ujumla
kuacha tabia ya kueneza habari sizizokuwa za kweli” Amesema Kamanda Kamugisha.
Aidha Kamanda Kamugisha
amesema kuna malalamiko yanayotolewa kuhusu Jeshi la Polisi mkoani hapo
kujihusisha na ulanguzi wa bidhaa zinazouzwa kwenye kanteeni za Polisi, taarifa
hizo ni za uongo kwani Serikali imeshafuta msamaha wa kodi katika bidhaa hizo
ambazo zilikuwa na bei tofauti na zile zilizopo katika maduka ya kiraia.
Jeshi la Polisi ni
chombo cha ulinzi na usalama wa raia na mali zake hivyo wananchi wanatakiwa
kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kupamabana na uhalifu uliopo.
Post a Comment