Makamu wa pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Akutana na Rais Magufuli leo Ikulu.....Amhakikishia Kuna Amani Zanzibar na Wanasubiri Tarehe ya Uchaguzi itangazwe
mwambawahabariblog
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali
Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibar wanasubiri
kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.
Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 20
Januari, 2016 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais
"Mimi nimekuja kumpa taarifa juu ya hali yetu Zanzibar inavyokwenda,
nimemueleza kwamba Zanzibar ipo salama, Zanzibar ina utulivu na ina amani,
nimeona nije nimueleze kwa kuwa yeye ni kiongozi wetu"alisisitiza Balozi Seif Ali
Idd.
Makamu huyo wa pili wa Zanzibar ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa
amani na utulivu, wananchi wa Zanzibar wanaendelea na shughuli zao kama
kawaida tofauti na inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hayo yanayoandikwa kwenye magazeti kuwa Zanzibar kuna fujo, Zanzibar
kutatokea machafuko sio kweli, na kama unavyojua uchaguzi ulifutwa na tume ya
uchaguzi na tunasubiri tarehe mpya ya uchaguzi itangazwe na tume ili tufanye
uchaguzi" amebainisha Balozi Seif Ali Idd.
Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
Post a Comment