Ads

TFDA YATOA SOMO KUHUSU MATUMIZI A CHAKULA SALAMA

mwambawahabariblog                                                                


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhamasishaji wa masuala ya Chakula Salama iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam


WANANCHI wameshauriwa kuangalia usalama wa chakula ili kuweza kuepuka vimelea vya viini vya magonjwa yanayotokana na kula chakula kisicho salama.


Ushaurihuo umetolewa  na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakulana Dawa (TFDA)  bw Hiiti Sillo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhamasishaji masuala ya usalama wa Chakula, amesema kula chakula chenye usalama  inafanya jamii kuwana afyabora nakufanya  taifa kuwa nanguvu kazi na maendeleo kiuchumi.
Amelisema kuwa chakula ni muhimu kwa maisha ya binadamu kwa kula chakula ambacho hakijachafuliwa na viini vya magonjwa kama, kuhara,kipindupindu homa ya matumbo.

Sillo alisema kwamujibu wa shirika la afya duniani,  watu milioni 91 duniani wanaugua magonjwa kutokana na kula chakula kilichochafuliwa na viini vya vimelea magonjwa.

Amelisema TFDA licha kuwa na changamoto lakini wameweza kuwa na mafanikio kwa kuweka watendaji mipakani pamoja na viwanja vya ndege na bandari wa kufanya ukaguzi wavyakula vinavyoingizwa  nchini.


No comments