Ads

Baraza la Mitihani ( NECTA ) Latangaza Matokeo ya Darasa la Nne....... Bofya Hapo chini kuyaona

mwambawahabariblog

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya 

kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi 

wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo 

iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza 

hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika 

kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 

waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 


108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.

Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 

89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi 

waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.

==>Bofya Hapa Kuyaona Matokeo

No comments