Rais Dkt. Magufuli Amteua Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.
mwambawahabariblog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (Chancellor of the University of Dar es salaam).
Rais Mstaafu Kikwete anachukua nafasi hiyo, iliyoachwa wazi na Marehemu
Balozi Fulgence Kazaura aliyefariki dunia Februari, 2014.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Ikulu Jijini
Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 17 Januari, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
21 Januari, 2016.
Post a Comment