TFF YATAKIWA KULIPA KODI
Na,Said Ali
Serikali imelitaka shirikisho la soka nchini TFF kulipa kodi kwakuwa mpango huo ni kanuni na moja ya
sheria ya nchi ili kusaidia kuleta maendeleo ya soka hapa nchini.
sheria ya nchi ili kusaidia kuleta maendeleo ya soka hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo na Henry Lihaya ambae ni Katibu Mkuu wa Baraza
la michezo Tanzania BMT wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa pili wa
bodi ya ligi TPLB, amesema kwamba kutokana na maagizo ya rais wa
jamhuri ya muungano wa tanzania Dk John Pombe Magufuli kuwa ni wajibu kwa kila
taasisi kulipa kodi.
Hata hivyo ameweza kuwatoa hofu viongozi wa shirikisho kuwa serikali
itasimamia maendeleo ya soka ktk maeneo mbalimbali ili kusaidia shirikisho hilo kufanikisha kupata vifaa ambavyo vimekwama bandarini kutokana na kushindwa kulipiwa kodi zikiwemo nyasi bandia.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Ahamad Yahaya amesema kuwa ameiomba serikali kupitia kodi ambayo wanakusanya katika maeneo ya michezo iweze kuelekezwa katika michezo ili kuviokoa vilabu ambavyo vinashindwa kujiendesha.
aidha amesema kwamba kwa sasa kodi ambayo inakusanywa viwanjani haipelekwi
sehemu husika hivyo wanaiomba serikali iweze kuingilia kati ili maendeleo ya soka yazidi kuendelea.
Post a Comment