Na John luhende
Mwamba wa habari blog
 |
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye [ katikat]i ,kulia ni Naibu waziri wake Mh,Annastazia Wambura [aliyesimama] ni Olegabriel Elisante Katibu Mkuu wa wizara hiyo, akiwakaribisha wizarani hapo.[Picha na John Luhende ]Add caption |
Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, wametakiwa kuwa na nidhamu na
kuheshimiana kwa wakubwa na wadogo,mfanyakazi wa chini hadi ngazi za juu ili
kuleta ufanisi na kuendana na kasi ya serikali ya awamu
ya tano.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye wakati akizungumza na
wafanyakazi wa wizara hiyo makao makuu katika hafla ya kumkaribisha ofisini
kwake baada ya kuteuliwa na rais Dk. M agufuli na kuwaomba watumishi wote kumpa
ushirikiano yeye pamoja na Naibu wake.
Aidha Nape
amesema kuwa wizara hiyo imekuwa ikipatiwa bajeti ndogo ukilinganisha na ukubwa
wa majukumu yake na amehaidi kuipigania bajeti hiyo iongezwe ili iweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Post a Comment