Ads

Wizara ya nishati na madini yazindua mfumo mpya wa malipo ya leseni za madini

Kamishna msaidizi wa madini kitengo cha leseni John Nayopa Akizungumza na waandishi wa habari.picha na John Luhende.

Na Jesca Mathew 
mwambawahabariblog 
Wizara ya nishati na madini imezindua mfumo wa malipo ya ada za leseni za madini kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transaction Portal [OMCTP] ambao utaanza kutumika kwa mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 10  Desemba 2015.

  1. Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna Msaidizi wa madini kitengo cha Leseni Bwana John Nayopa amesema kuwa mfumo huo utaweza kupunguza tatizo la mlundikano wa maombi ya leseni za madini kwenye ofisi za madini pamoja na kuongeza uwazi na kasi ya utoaji wa eseni za madini


Aidha amesema kuwa mfumo huu ni rahisi Zaidi na wa haraka hivyo amewataka wachimbaji wadogo wadogo kutumia mfumo huo ili waweze kupata huduma kwa wakati kwa kuwa mfumo huu utahusisha mitandao ya simu.

Bw. Nayopa ameongeza kuwa hadi sasa leseni 5919 zimesajiliwa ambapo pia kuna maombi 117 na leseni za utafutaji leseni za uchimbaji mkubwa na wa kati zilizosajiliwa ni 111 pamoja na leseni hai za uchimbaji mdogo zilizosajiliwa kwenye huduma hiyo ni 2,593 huku jumla ya kampuni hai 370 zimesajiliwa.

Hata hivyo wizara inawakumbusha wateja wote kuwa ili kujisajili kwenye mfumo huo wa OMCTP wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo;

Fomu ya kuomba usajili wa OMCPT iliyojazwa kikamilifu.


Leseni halisi pamoja na stakabadhi za malipo ya leseni husika kutokea leseni husika ilipohusishwa kwa mara ya mwisho hadi wakati wa kuomba usajili. 

Kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa habari maelezo Vicent Tiganya.Picha na John Luhende



No comments