Ads

MAKAMPUNI YA WAKWEPA KODI YAJISALIMISHA TRA


(picha na mtandao)

MAKAMPUNI 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku saba za msamaha wa Rais wajamhuri ya muungano wa Tanzania Dr  John Pombe  Magufuli.


Deni la kodi inayodaiwa kwa makampuni hayo ni Sh bilioni 3.75, hivyo  wamiliki watachukuliwa hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango  wakati  akielezea makusanyo ya kodi ya makontena toroshwa katika bandari kavu ya Azam, kinyume cha sheria pamoja na kumalizika kwa muda wa siku saba ulio tolewa na Rais Magufuli kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi waliyokwepa, bila kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

 Mpango aliongeza kuwa siku hizo saba zimelikia kikomo juzi, hivyo hatua kali za kisheria kwa wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi katika kipindi hicho zinafuata .

"Tumewasihi waje kulipa kwani huruma ya Rais sasa imeisha... tulifanya uhakiki na kuthibitisha kuwa kampuni hizo zipo. Wamekuja kulalamika lakini hakika hakuna atakayesamehewa kulipa,   sheria sasa itabidi ifuate mkondo wake "


Alitaja kampuni hizo kuwa ni Ahmed Saleh Tawred anayedaiwa Sh milioni 59.23; Cla Tokyo Limited Sh milioni 77.52; Farida Abdullah Salem Sh milioni 75.33 na Juma Kassem Abdul Sh milioni 190.18.

Wengine ni Libas Fashion Sh milioni 52.94; Rushy Wheel Tyre Center Co Ltd, Sh bilioni 1.8; Said Ahmad Hamdan Sh milioni 68.36; Said Ahmed Said Sh milioni 68.73 na Salum Continental Co Ltd Sh milioni 151.17.
 Pia yumo Salum Link Tyres Sh milioni 343.44; Simbo Yonah Kimaro, Sh milioni 69.22; Snow Leopard Building Material Co Ltd Sh milioni 93.97; Swaleh Mohamed Swaleh Sh milioni 34.68; Tybat Trading Co Limited, Sh milioni 598.69 na Nasir Saleh Mazrui Sh milioni 70.10.

 Mpaka kufikia jana TRA walikuwa wamekusanya Sh bilioni 10,643.004,948.46 kutoka kwa kampuni 28 ambapo kampuni 13 zimelipa kodi yote iliyokadiriwa, ambayo ni Sh 4,167,130,173.89 na Sh 2,303,637,554.57 kutoka kampuni 15 zilizolipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa.

Dk Mpango alisema Sh bilioni 4.17 zimelipwa na kampuni ya Azam ICD, ikiwa ni dhamana ya kodi iliyokwepwa, hivyo atatakiwa kumaliza kulipa kodi yote inayodaiwa kwa mujibu wa nafasi yake kama mwenye dhamana.

Alisema wakati utekelezaji huo ukiendelea, ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo ya makontena yaliyoondolewa bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha, TRA imefungua akaunti maalumu katika Benki Kuu yenye namba 9921169785 inayoitwa Commissioner for Customs and Excise – Container Account.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, mpaka sasa watumishi 36 wa TRA wanaotuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na makontena hayo kuondoshwa bandarini.


Aidha, alisema TRA imepata taarifa zisizopungua 15 kutoka kwa wananchi kuhusu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi na walipakodi wanaokwepa kodi.
Aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa na kuwaomba wengine wajitokeze kutoa taarifa zaidi na mamlaka hiyo inawahakikishia kuwa itawalinda   alisema mpango na kuongeza kuwa sasa wanafanya utaratibu wa kupata mashine za kupiga picha za ziada.

Na: Mwambawahabari blog

No comments