JESHI LA POLISI LAJIPANGA KUIMARISHA USALAMA SIKUU
Msemaji wa jeshi la Polisi nchini, SSP Adivera Bulimba |
Na John Luhende
mwambawahabari
Katiki kipindi hiki kuelekea sikukuu za mwisho
wa mwaka Jeshi la Polisi nchini limesema limejipanga kufanya operesheni kali ya
kukamata madereva wasiofuata sharia za
usalama barabarani ikwa nipamoja na pikipiki kubeba abiria Zaidi ya mmoja
(mishikaki) magari kuzidisha abiria,kwenda mwendo kasi ulevi wakati wakuemdesha chombo cha moto na
uzembe mwingine utakaofanywa na madereva.
Akizungumza
na waandishi wa habari msemaji wa jeshi
la polis nchini SSP Advera Bulimba aliesema jeshi la polisi lina wataka wananchi kote
nchini kuwa makini na kuchukua hatua
stahiki za haraka pindi wanapo ona viashiria vyovyote vya uvunjifu wa Amani katika
maeneo yao na sehemu mbali mbali za maeneo yabiashara
Aidha Advera aliwataka wamiliki wote wa kumbi za starehe
kuzingatia uhalali wa matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu ili
kuendana na uwezo wa kumbi hizo badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi, na ameongeza kuwa wananchini watumie vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha na usambazaji wa taarifa
za uchochezi uongo na upotoshaji kwa jamii vikiwemo utapeli
Post a Comment