SERIKALI YATATUA MGOGORO WA TIMU YA SOKA STAND UNITED YA SHINYANGA
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari(picha na John Luhende)
Na John Luhende
mwambawahabariblog
Serikali imeagiza kumalizika kwa mgogoro
uliopo baina ya Timu ya mpira wa miguu ya Stand United na Kamati ya uendeshaji
wa timu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Agizo hilo limetolewa leo
jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Moses Nnauye mara baada ya kumaliza kikao na uongozi na Stand United.
Amesema
kuwa imefika wakati vilabu vipewa uhuru
wa kujiendesha kwa kutumia katiba zao badala ya kuingiliwa na chombo kingine
chenye maslahi yake binafsi.
“Wizara itasaidia kuona mgogoro huu unaisha kwa Stand United
kupewa uhuru wa kujiendesha yenyewe na uongozi uliokuwapo kupewa mamlaka yake
ya kusimamia na kuendesha shughuli za Timu yao kwa mujibu wa Katiba”alisema
Nape
Aidha aliongeza kuwa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusimamia uendeshaji wa mchezo wa mpira wa
miguu kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za mchezo huo ili kuepuka
migogoro isiyokuwa ya lazima
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Timu ya Stand United Bw. Aman Vicent ameishukuru Serikali kupitia Wizara yenye
dhamana na masuala ya michezo kwa kuona umuhi wa kushughulikia na kumaliza
mgogoro huo unao athili club hiyo
Aman amesema kuwa kutokana na
makubaliano waliyofikia katika kikao hicho imani yao ni kuwa suala hili
litamalizika mapema kwa kuwa Waziri mwenye dhamana ameonyesha nia na utayari wa
kuhakikisha suala hili linaisha kwa wakati ili Timu iweze kusonga mbele kimichezo
Post a Comment