Ads

CRDB Kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar .



Dar es salaam 

Benki ya CRDB imeahidi kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar kuimarisha uwezo wa kifedha wa taasisi za umma, kuongeza tija katika matumizi ya mali na kuvutia uwekezaji wenye manufaa kwa uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Dkt. Abdullmajid Nsekela, amesema benki hiyo inalenga kufanya tathmini ya uwezo, mali na fursa zilizopo katika taasisi za umma ili kubuni suluhisho endelevu za kifedha na kibiashara.

Amesema ushirikiano huo hautalenga mikopo pekee, bali pia ushauri, uwekezaji, matumizi bora ya mali na kuvutia mitaji.

“Tulisaini leo, lakini kazi inaanza leo. Hili jambo halitaishia kwenye kusaini mkataba.”

CRDB imesema inatarajia ushirikiano huo kuongeza uwekezaji, ajira, mapato ya Serikali na kuboresha huduma kwa wananchi.

Kwa upannde wake Msajili wa Hazina Zanzibar, Waheed Ibrahim Muhammad Sanya, ameishukuru CRDB kwa ushirikiano huo, akieleza kuwa mchakato wa kufikia makubaliano hayo umechukua muda na sasa umefikia hatua ya utekelezaji.

Ameongeza kuwa Ushirikiano kati ya CRDB Bank na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar umeingia hatua muhimu, ukilenga kuimarisha utendaji na ufanisi wa taasisi mbalimbali za umma.

Amesema ushirikiano huo utasaidia kutafuta njia bora za kuziimarisha taasisi zinazohusika na biashara, elimu, afya na huduma nyingine, huku Serikali ikiahidi kushirikiana na CRDB kuhakikisha makubaliano hayo yanazaa matokeo chanya.

" Lengo ni moja: kuona taasisi za umma Zanzibar zikifanya vizuri zaidi na kutoa huduma bora kwa wananchi" Amesema  Msajili. 

No comments