OPERESHENI MAALUMU YA BODA BODA NA BAJAJI KUANZA LEO
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limeanza leo, Septemba 29, 2026, operesheni maalumu ya nchi nzima kuwabana waendesha boda boda na bajaji wanaokiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.
Operesheni hiyo inalenga kuongeza utii wa sheria na kupunguza makosa yanayoweza kusababisha ajali, majeruhi na vifo.
Miongoni mwa mambo yatakayokaguliwa ni: Matumizi sahihi ya kofia ngumu
Idadi ya abiria
Utaratibu wa kukaa ndani ya bajaji
Makosa mengine ya usalama barabarani
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP William Mkonda, ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya madereva wa pikipiki na bajaji pamoja na viongozi wa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.
Madereva, zingatieni sheria za usalama barabarani.
#BodaBoda #Bajaji #UsalamaBarabarani #PolisiTanzania #DarEsSalaam Tanzania Habari BreakingNews TrafficPolice

Post a Comment