LATRA YAIMARISHA UDHIBITI WA MADEREVA
Na . Hashim Mushi
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini, LATRA, imeendelea kuimarisha udhibiti wa madereva wanaotoa huduma za usafirishaji kwa kuhakikisha wanathibitishwa na kufikia viwango vinavyotakiwa.
Akizungumza kuhusu hatua hizo, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Dkt. Habibu J. Suluo, amesema kwa mujibu wa sheria, mamlaka hiyo ina jukumu la kuthibitisha madereva na kusajili wahudumu wanaofanya kazi katika sekta ya usafirishaji.
Amesema dereva anayehitaji kuthibitishwa na LATRA anatakiwa kufanya mtihani maalumu wa mamlaka hiyo, ambao ni tofauti na mitihani inayofanywa na vyombo vingine, ikiwemo Jeshi la Polisi na vyuo vya udereva.
Dkt. Suluo amesema utaratibu huo umewekwa ili kuhakikisha dereva anayekabidhiwa jukumu la kuendesha gari la huduma za usafirishaji anakuwa na sifa na uelewa unaohitajika.
Amesema mtihani huo una maswali 100 na hufanyika kwa kutumia kompyuta, huku majibu yakisahihishwa kupitia mfumo wa kielektroniki.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na LATRA, mwaka wa fedha 2022/2023, watu 177 walifanya mtihani huo.
Idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi kikubwa, ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026, watu 6,356 walifanya mtihani huo.
Kwa ujumla, watu 15,547 wamefanya mitihani ya kuthibitishwa na LATRA tangu kuanza kwa utaratibu huo, ambapo watu 8,642 walifaulu, sawa na asilimia 56 ya waliofanya mtihani.
Dkt. Suluo amesema katika mwaka wa kwanza, kati ya watu 177 waliofanya mtihani, 161 walifaulu.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2025/2026, kati ya watu 6,356 waliofanya mtihani, watu 4,079 walifaulu, sawa na takribani asilimia 64.
Amesisitiza kuwa dereva ambaye hafanyi au hafanikiwi katika mtihani huo hawezi kupewa uthibitisho wa LATRA unaomwezesha kuendesha gari linalotoa huduma za usafirishaji.
Kwa hatua hiyo, LATRA inalenga kuhakikisha madereva wanaoendesha mabasi, malori na magari ya kukodi wanakuwa na sifa na uelewa unaohitajika kwa usalama na ufanisi wa huduma za usafirishaji. Ongeza kuwa alikuwa wazungumza katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri LATRA ukioandaliwa na OFISI ya Msajili wa hazina

Post a Comment