Ads

Agricom Africa Yawezesha Wakulima Kupata Zana Bora za Kilimo

 



Salvator Chengula, Afisa Masoko wa Agricom Africa Limited, amesema kampuni hiyo inalenga kumpa mkulima suluhisho kamili kwa kuhakikisha anapata zana bora na imara za kilimo.

Amesema Agricom Africa inashirikiana na wazalishaji mbalimbali wa mashine za kilimo, wakiwemo Field King, Kubota, Swalaj na Lovol, ili kuwapatia wakulima zana zinazokidhi mahitaji yao.

Chengula amesema changamoto kubwa kwa wakulima, hasa wadogo na wanaoanza kilimo, ni uwezo wa kumudu gharama za mashine hizo. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Agricom Africa imeungana na zaidi ya taasisi 11 za kifedha, zikiwemo benki, zinazowezesha wakulima kupata mikopo ya kununua zana za kilimo kwa masharti nafuu.

Amesema baadhi ya taasisi hizo hutoa mikopo kwa mkulima mwenye uwezo wa kulipa kianzio cha kuanzia asilimia 10. Kwa mfano, mashine yenye thamani ya Sh milioni 100 inaweza kupatikana kwa kianzio cha Sh milioni 10, huku masharti mengine yakihitaji kianzio cha hadi asilimia 25.

Aidha, Agricom Africa hutoa huduma ya udhamini (warranty) kwa kipindi cha miaka miwili, ikiwemo matengenezo ya mashine pale inapoharibika. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mkulima anatumia mashine yake kwa ufanisi wakati wote na kupata nafasi nzuri ya kurejesha mkopo bila usumbufu.

Kwa huduma hizo, Agricom Africa inalenga kuwawezesha wakulima wadogo na wakubwa kupata zana bora za kilimo na kuongeza uzalishaji wao.

No comments