Ads

VIONGOZI WA WILAYA YA ILALA NA HALMASHAURI YA JIJI LA DA ES SALAAM WAWATEMBELEA WAJASILIA MALI SABA SABA

 


Mwamba wa habari

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema bidhaa zilizooneshwa na wajasiliamali wa  jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla hususani zinazouzwa katika  maonesho Maonesho ya 50 ya Biashara ya kimataifa yanayo endelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Kilwa road Dar es salaam, zimeonesha ubora mkubwa na zina uwezo wa kushindana na bidhaa kutoka nje ya nchi.


Amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga zaidi ya Shilingi  bilioni 22 kwa ajili ya mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali, huku akiwataka wananchi kutumia fursa hiyo kukuza biashara  kupitia mikopo hiyo.


“Leo tumejionea  bidhaa ambazo unaweza kuzipeleka supermarket yoyote na zikashindana na biashara yoyote au bidhaa yoyote kutoka nje ya Tanzania,” amesema.

Aidha amesema , Serikali imeendelea kuweka mazingira ya kuwawezesha Watanzania kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, ambapo kila mwananchi anapaswa kuwa na nafasi ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Da es salaam Nurdin Bilal akizungumza wakati wa ziara  hiyo ya viongozi wa Wilaya ya Ilala na Halmashauri ya Jiji , amesema Mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambayo ni asiliama 10 imeatajwa kuonesha matokeo baada ya baadhi ya wanufaika kutumia fedha hizo kuanzisha viwanda vidogo na kupanua uzalishaji wa bidhaa zao.

Amesema baadhi ya vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo vimeweza kupiga hatua kubwa kiuchumi, huku vingine vikifikia hatua ya kuanzisha viwanda vidogo baada ya kupata fedha za kuwawezesha kuongeza uzalishaji.

“Tumeshuhudia kuna vikundi pale vimeanzisha mpaka viwanda vidogo vidogo na vimepata zaidi ya Sh milioni 80 za kuendelea. Wengine wamepata milioni 30 na huu ni mfano tu, wapo wengi wa aina hiyo,” alisema.

Alisema mafanikio hayo yanaonesha kuwa mikopo hiyo si suala la maneno pekee bali ni chachu ya kuwawezesha wananchi kujenga shughuli zao za kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Elihuruma Mabelya amesema mikopo hiyo ni chachu ya maendeleo  na imesaidia kuinua uchumi katika jamii









No comments