WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA OFA ZA TTCL SABASABA 2026


Na Mwandishi Wetu
Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Banda Janeth Maeda amesema ushiriki wa Shirika katika Sabasaba 2026 unalenga kuwasogezea wananchi huduma, kuongeza uelewa kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na TTCL, pamoja na kujenga mahusiano imara na wateja na wadau mbalimbali.
Aidha, amebainisha kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa Shirika kupokea mrejesho wa wateja ili kuendelea kuboresha huduma na kuendana na mahitaji ya soko la mawasiliano linalobadilika kwa kasi.

Aidha,wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kutumia buree public Wi-Fi inayopatikana katika viwanja hivyo ili kufahamu speed ya intanet ya TTCL.
TTCL inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Shirika hilo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ili kujionea teknolojia bunifu, kupata elimu kuhusu huduma za mawasiliano na kunufaika na ofa maalum zinazopatikana katika kipindi chote cha maonesho.

Post a Comment