DAYOSISI ya Mashariki lawataka Vijana kujitokeza Katika Tamasha la Twenzetu kwa Yesu
DAYOSISI ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la kiinjili la Kilutheri Nchini limewataka Vijana kujitokeza Katika Tamasha la Twenzetu kwa yesu linalotarajiwa kufanyika juni 13 Mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Peckers jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jan Naibu Katibu Mkuu DMDP Mchungaji Wilbrod Masai amesema kuwa Tamasha hilo linalotarajiwa kuhudhuliwa na watu takriban 35000 linalenga kuwa jengea Vijana Uchaji wa Mungu.
"Tamasha hili lenye kauli mbiu Be the star kuwa kijana mwenye Baraka kwa Mungu naMachoni Mwa watu"Amesema Naibu Katibu Mkuu DMDP Dk.Willbroad Masai DK.Masai .
Ameongeza kuwa katika Tamasha hilo kutakuwa na kwaya 5 na waimbaji mbalimbali Baadhi yao nipamoja na Boaz Darnken,Praise Team Kibangua ambapo Tamasha hilo linaongozwa na Neno la Mungu kutoka yohana 8:31
Aidha kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mission na Uinjilisti DMDP Henry Mwinuka amesema Hali ya Usalama katika Tamasha hilo ni yakutosha. Amesema Tangu Tamasha hilo lianze limesha hudhuriwa watazamaji 5000.
Post a Comment