Ads

John Mabagala azungumzia mchakato Usafirishaji Soko la Kahawa Nchini

Na Francisco Peter , Dar es Salaam

Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) pamoja na wadau wamekaa kikao cha pamoja kufanya tathimini ya zoezi la uandikishaji wa dafutari la taifa la wakulima wa Kahawa nchini.

Ambapo umoja wa ulaya unaendesha mpango ambao unatekelezwa na serikali kuhakikisha kahawa zinazoingia ulaya hazitokani na uharibifu wa mazingira katika mchakato wa uzalishaji.

Kwa mujibu wa bodi ya Kahawa nchini Tanzania inasafirisha Kahawa zote kati ya asilimia 60 hadi 70 kwenye Kahawa zote zinazosafirishwa nchini.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa EUDR, Bw. John Mabagala kutoka taasisi ya Emergency Marketing International (EMI), amesema nchi za  Ulaya zimeunda sheria ambayo inataka lazima kuwe na dafutari maalum linaloonesha Taarifa ya mashamba ya wakulima yapo maeneo yapi.

"Ambapo kujua maeneo hayo inasaidia kuona mahali ulipo uharibifu wa mazingira,"amesema.

Mabagala amesema kuwa tayari wameweza kuona usajili wa wakulima 150 katika Mkoa miwili ya Kagera na Songwe ambapo kwa kuanzia wamefikia mashamba 200, 000 .

Katika kutekeleza majukumu yake pia TCB ni chombo kikuu cha udhibiti na kinacho -hakikisha kuwa wadau wote katika mnyororo wa thamani wa kahawa wanazingatia Sheria ya Tasnia ya Kahawa, kanuni zake pamoja na viwango vinavyotumika kitaifa, kikanda na kimataifa. 

Aidha, Bodi inakuza uwazi, ufanisi, uhakika wa ubora na ushindani katika sekta ya kahawa, huku ikiendeleza maendeleo endelevu ya mnyororo wa thamani na kupanua fursa za masoko ya kahawa ya Tanzania ndani na nje ya nchi.

TCB inaendelea kujenga sekta ya kahawa iliyo shindani, jumuishi na endelevu, inayochangia ukuaji wa uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wakulima wa kahawa.





No comments