Ads

Naibu Meya John Ryoba achangia shilingi milioni 1. KKKT Ushirika wa yombo




Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)

Naibu meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam John Ryoba Mrema, amechangia shilingi milioni 1 kwaya ya KKKT Ushirika wa yombo Kiwalani wilaya Ilala. 


Naibu meya John Ryoba Mrema mchango huo Dar es Salaam katika ibada Maalum ya uzinduzi wa album ya tano ya Kwaya ya uinjilisti KKKT Tumain Usharika wa Yombo


"Kwa niaba meya nalipongeza Kanisa hili KKKT kwa malezi mazuri kwa vijana  na kuweka makundi ya vijana na Wazee katika kwaya naomba waumini wa Kanisa la KKKT Ushirika wa yombo tuombee Amani Taifa letu kutokana na vita vinavyoendelea mashariki ya kati"alisema John Ryoba. 


Naibu Meya John Ryoba, aliwataka waumini wa kanisa hilo kumiombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais ,Waziri Mkuu kwa kuwaongoza Watanzania.


Alisema kutokana na vita vinavyoendelea mashariki ya kati mpaka vimepelekea mfumuko wa bei ya mafuta kuwa kubwa  aliwataka Watanzania kuwa na subira bei ya mafuta itashuka baada vita kumalizika.


Kwa upande wake Mwalimu wa kwaya Ushirika wa yombo KKKT Anania Joel Duma, alisema Mpaka sasa wamezindua album ya tano zenye nyimbo za kisasa ukiingia katika YouTube ushirika wa Yombo unazikuta .


Mwana kwaya Anistiani Anania Juma, alimpongeza Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam John Ryoba Mrema kwa mchango mkubwa aliochangia kwaya kwaya hiyo ambapo alisema kazi ya kutangaza Injili endelevu ukiwa na Mungu ndani ya moyo wako amani itaimalika 

No comments