Ads

Waziri Dkt Dorothy Gwajima ashiriki Mbio za Marathoni na (TWCC)

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi MaalumMhe. Dkt Dorothy Gwajima  ameishiriki mbio za marathoni zilizoandaliwa na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) ambayo imeadhimisha  miaka 20.

Akizungumza kupitia Maadhimisho hayo  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam , Dkt Dorothy amesemakuwa chemba hiyo imekuwa ndiyo kisima cha kujifunza kufikia maendeleo kuanzia biashara ndogondogo za kati  hadi  uchumi mkubwa.

"Kupitia chemba hii inawezesha muungano wa safari ya kuwezesha wanawake kiuchumi kuimarisha mitandao ya kibiashara na kufungua milango ya masoko ndani na nje ya nchi ,"amesema Dkt Dorothy.

Dkt. Dorothy amesema kuwa kupitia jukwaa hilo wanawake wameweza kuunganishwa katika fursa kwenye taasisi mbalimbali.

Waziri huyo amesema kuwa serikali itashirikiana vema na chemba hiyo ilikuwezesha kujua fursa mbali mbali na kusisitiza wanawake kuwa wakwanza kukataa vitu vinavyo sabsbisha mmomonyoko wa maadili.

Aidha amesema maelfu ya wanawake wameweza kusajiliwa na kukuza kipato chao na kuchangia kiasi kikubwa katika Pato la taifa.

Pia katika maadhimisho hayo ya miaka 20 ya chemba hiyo ya wanawake nchini  yaliyoambatana na mbio za marathoni ,Waziri ametoa zawadi mbalimbali kwa washiriki wa mbio hizo zikiwemo medali.

Imeelezwa kuwa kupitia mbio hizo  maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila ushiriki wa wanawake katika nyanja mbali mbali.

Uwezeshaji wanawake kiuchumi  ni kiaumbele hivyo mbio walizokimbia ni zaidi ya mashindano ni ishara ya mwanamke anayeitaji mitaji kukuza biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Biashara Tanzania TWCC, Dkt. Mwajuma Hamza amewashukuru wazamini  wote katika kufanikisha shughuli hiyo.

No comments