D Voice acha tu ,baada ya Idd kushikilia anga lote ; Msanii yeyote asiyesikia atapotezwa
Na Francisco Peter Dar es Salaam
Msanii nyota hapa nchini kupitia ngoma zake zinazoendelea kufanya vema kwenye muziki wa singeli D Voice ametangaza ziara itakayoanza na Mkoa wa Mwanza.
Mapema tu amewatishia wasitoe nyimbo yeyote kwani wasipo sikia, wanakwenda kufanya uwekezahi wenye hasara za kimuziki.
" Nataoa taarifa muda unaongea kwani katika kipindi hicho nakwenda kufanya balaa katika singeli nimeamua nakwenda kufanya makamuzi na kuhakikisha muziki huo unakwenda levo kubwa zaidi,"amesema D Voice.
Nyota huyo tayari amepewa gari itakayorahisisha makamuzi yake huku akianzia Mkoa huo wenye samaki wengi aina ya sato na sangara.
D Voice kutoka lebo namba moja ya burudani Afrika ya Mashariki WCB,D amekabidhiwa gari na kampuni ya Kwanza Oil ambayo ataitumia katika tour yake katika Mikoa 15 hapa nchini.
Tour hiyo ambayo ameipa jina la D Voice tour 2026 itaanza katika Mikoa 10 kote nchini Tanzania na baadaye kwenda katika nchi mbalimbali Afrika Mashariki inatajwa kama tour kubwa kuwahi kufanywa na msanii wa Singeli hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla fupi ya kukabidhiwa gari hilo iliyofanyika March 18,2026 Jijini Dar es salaam.
Msanii D Voice ameishukuru kampuni ya Kwanza Oil kwa Kudhamini matamasha yake ya muziki ambayo atayafanya hapa nchini akianzia Kanda ya ziwa katika Jiji la Mwanza huku akiahidi kutoa zawadi mbalimbali za mafuta kwa akina mama katika Kila Mkoa atakaopita.
Amesema kukabidhiwa gari hilo ni ishara kwamba kampuni ya Kwanza Oil imeamua Kudhamini harakati za kuutangaza muziki wake kwa mashabiki zake kote nchini ili kuendelea kuijenga ngome yake kama msanii namba moja wa singeli Tanzania.
"Mimi kwa sasa sihitaji tena ufalme wa muziki wa singeli nimewaachia wengine mimi ndiyo rais wa singeli na kwa kuwa sisi hatuongozwi na ufalme,rais ndiye mwenye madaraka makubwa kuliko wote hivyo Mimi ndo rais wa singeli Tanzania ndo maana kampuni ya Kwanza Oil imeamua kushirikiana nami" alisema D Voice
Kwa upande wake msemaji wa kampuni ya Kwanza Oil Khalfan Ramadhan amesema wao kama kampuni ya utengenezaji wa mafuta bora ya alizeti hapa nchini wameamua kumkabidhi gari hilo msanii huyo kama ishara ya kuunga mkono tour yake hapa nchini kwani ni msanii bora anayefanya vizuri kwa sasa.
"sisi kama kampuni bora ya utengenezaji wa mafuta ya alizeti yenye ubora Tanzania nzima tumeamua kushirikiana na msanii D Voice pia ili kuitangaza kampuni yetu ambayo imeleta sokoni bidhaa bora ya mafuta yasiyo na cholesterol kwa bei nafuu kwa watanzania" alisema msemaji huyo
Aidha ameongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za wasanii na sekta ya michezo ili kukuza sekta hizo ambazo zinalitangaza vyema Taifa la Tanzania kimataifa.
Tour ya hiyo ya mkali huyo wa singeli kutoka lebo ya WCB inatarajiwa kuanzia katika Jiji la Mwanza baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan na kupita Mikoa mbali mbali nchini na baadaye kumalizia katika Jiji maarufu kwa utalii duniani ambalo liko katikati ya bara la Afrika yaan Arusha kabla ya kwenda katika nchi nyingine Afrika Mashariki.

Post a Comment