Watanzania Watakiwa Kujifunza Urithi wa Ukombozi wa Afrika.
Akizungumza wakati wa kufungua mdahalo uliofanyika katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa, Dkt. Julieth Kabyemela, amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi yenye kumbukumbu nyingi kuhusu harakati za ukombozi barani Afrika.
“Sisi kama Watanzania, siku hii ni muhimu sana kwetu, kwa sababu nchi yetu ilikuwa kitovu cha harakati za kupigania uhuru wa mataifa mbalimbali ya Afrika,” amesema Dkt. Kabyemela.
Naye Mratibu wa Kituo hicho, Christopher Mhongole, amesema kuwa nchi nyingi za Afrika zinaweza kujifunza historia ya ukombozi kwa ushahidi wa kutosha kwa kuitembelea Tanzania, ambako harakati nyingi ziliratibiwa.
“Hivyo basi, maadhimisho kama haya ni muhimu kwa Tanzania, kwani hutoa fursa ya kuielimisha jamii, hasa vijana, ili watambue na kuthamini historia ya nchi yao,” amesema Mhongole.
Aidha, mmoja wa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari Zanaki, jijini Dar es Salaam, Jesca Denis Monahera, aliyeshiriki katika mdahalo huo, amesema kuwa jambo la kwanza alilojifunza ni umuhimu wa kuwa mzalendo kwa nchi yake.

Post a Comment