AMANI NITUNU KWA TAIFA LETU TUSIKUBALI MANENO YA KICHOCHEZI
Na mwandishi wetu
Tabora
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Maarifa,Kilimo na Nishati (MAKINI), Coaster Kibonde amewataka watanzania kudumisha amani iliyopo nchini kwamba Amani ya Taifa letu ni dhamana yetu sisi wenyewe,amani ikipotea hakuna pakuipata.
Akizungumza Leo Oktoba 8,2025 katika mkutano wa muendelezo wa kampeni Jijini Tabora amesema kuwa tulinde amani yetu tumeiasisi kutoka enzi na enzi za wazazi wetu amani ambayo duniani kote wanaionea wivu,choyo tuilinde, yeyote anayeonyesha maneno ya kichochezi Wala maneno ya kutugawa watanzania tumkatae.
"Amani ya Taifa letu ni dhamana yetu sisi wenyewe,amani ikipotea hakuna pakuipata,na waathirika wakibwa katika vita ni wanawake na watoto vijana naibrahisi kukimbia tusikubali kuharibu amani yetu,tuilinde amani yetu tumeiasisi kutoka enzi na enzi msishawishike Wala msidanganyike na wanaoleta uchochezi na ushawishi kwa ajili ya machafuko na ghasia",amesema
Amani ya nchi ndio dhamana ya mwananchi mwenyewe lakini wewe mwenyewe usishawishike kwa namna yetote ile kuvuruga amani ya Taifa letu.
Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura na kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mara baada ya kupiga kura kurudi nyumbani kwenda kusubiri matokeo
Pia amesema kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana Kuna watu ambao wanaposti matukio ya kutuchochea kwamba Oktoba 29 tuandamane"Mimi Coaster Kibonde ninawaomba muwapuuze hao watu kwa kuwa sisi watanzania Kila kukicha tunakwenda kutafuta mkate wa Kila siku kwa ajili ya familia zetu,je vita vikitokea mkate wako wa Kila siku utautoa wapi?tafadhali tuenzi amani yetu",
Amesema vipaumbe vya Chama chetu ni elimu,Kilimo na Afya na vinamlenga kila mwananchi wa Tanzania wa halI ya chini hadi juu ambapo amesema endapo atakuwa rais atahakikisha elimu inatolewa bure kuanzia elimu ya chekechea hadi chuo kikuu na wahitimu wa vyuo vikuu hawatakuwa tena na kurejesha mikopo Yao serikalini
Sanjari na hayo amesema kwamba atafanya mageuzi makubwa ya kiviwanda na viwanda hivyo vitazalisha Mali zinazohusiana na kilimo ikiwemo pembejeo hivyo pembejeo zitamsubiri mkulima
Sambamba na hayo,amesema kwamba atahakikisha mikopo ya asilimi kumi kwa wanawake ,vijana na makundi maalum itatoka kwa wakati na haitakuwa na masharti magumu .
Ameendelea kwamba atahakikisha Kila wilaya ya Mkoa wa Tabora kutakuwa na barabara za lami ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima kutoka shambani na pia atawatafutia wakulima masoko ya uhakika nje ya nchi.
Alieleza kwamba endapo atakuwa rais atahakikisha viwanja vya ndege vinaboreshwa na atanunua bombardier 70 ili kila mkoa ziweze kutua pamoja na nauli za usafiri huo zitashuka ili Kila mkulima aweze kupanda ndege
Alimalizia kwamba atahakikisha Kila mkoa Barabara zote zitajengwa kwa kiwango cha lami ili kurahisisha usafiri kwa wananchi
Post a Comment