ORYXY YASIMIKA MFUMO WA KISASA WA GAS , SOKO LA SAMAKI FERRY
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataita Ferry jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 21, 2025 katika soko hilo Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Albert Chalamila amesema agenda ya nishati Safi tangu Rais samia aizindue nchini kupitia mkutano wa Nishati Africa ulio husisha wakuu wa nchiza Africa umekuwa na faida kubwa na umeungwa mkono na wadu wa nishati.
Chalamila amesema matumizi ya nisahati safi umeleta tija kwa kuokoa Maisha ya akinamama ambao wengi waowalikuwa wanatumia nishati chafu ambayo ni hatari kwa afya.
Chalamila ametoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika uziduzi wa majiko ya nishati ya Ges katika Soko la Samaki Ferry Jijini Dar es salaam ambapo Zaidi ya majiko 48 yameunganishwa na mfumo wa watumiaji wakubwa wa Gesi kutoka Kampuni ya Oryxy Energies Tanzania .
Awali akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala mkoa wa Dar es salaam, Katibu tawala msaidizi Uchumi na uzalishaji Dkt Elizabeth Mshote, amesema takwimu zinasema Zaidi ya watu 33,000 hufa kila mwaka kutokana na matumizi ya nishati isiyo salama hapa nchini.
Aidha amesema katika taarifa za mkoa katika magonjwa Matano yanayo sumbua ni Pamoja na magonja ya mfumo wa upumuaji ambayo husababishwa na matumizi ya nishati chafu.
Hata hivyo amesema mkoa wa Dar es salaamu unaongoza kwa kuwa kinara kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo taasisi 552 kati ya 648 zinazotokana na jiji la Dar es salaam zimehamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia
Kwa upande wake Mhandisi Innocent Luoga kutoka wizara ya nishati , amesema tangu mkakati wa kitaifa wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia uzinduliwe Mei 8/2025 na Rais samia Suluhu Hassan , umeshuhudiwa uwekezaji kubwa kutoka sekta bibafsi, Serikali na wadua mbalimbali.
''Mkakati huu wa Miaka kumi unalenga kuhakikisha kuwa asilimi 80 ya watanzania wanahamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034"Amesema Luoga.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha hilo linatekelezwa taasisi zinazolisha watu wengi Zaidi ya miamoja kwa siku zinahamia katika matumizi ya nishati safi kupikia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Oryxy Gas , Benoit Araman, amewashukuru wadau wote waliohusika kwa namna mbalimbali katika kufanikisha kufikiwa uzinduzi wa Majiko hayo ya matumizi makubwa ya Gesi na kuongeza kuwa ni matokeo muhimu ya ushirikiano wa karibu na maandalizi ya kitaalamu na nidhamuya hali ya juu tangu utafiti, michora ya kihandishi hadi majiribio ya usalama.
Amesema faida za mfumo huo ni kuimarisha usalama ,hakuna hatariri kubwa ya uvujaji wa Gesi ,usalama ni wa hali ya juu na udhibiti wa dharura na umewekwa na wataalamu stahiki na ikitokea dharura mfumo huu una vifaa maalumu vya kuzima Ges isitoke na kufuata utaratibu wa usalama dhidi ya Moto.
Naye alikuwa Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Ilala Dar es Salaam Mussa Zungu, amesema awali wafanyabiashara wa soko hilo walimfikishia mahitaji yao hivyo aliwatafuta Oryx Gas na leo amefurahi kuona umefungwa mfumo huo ambao unakwenda kurahisisha shughuli za wafanyabiashara hao.
Kuzinduliwa kwa mradi huo utaimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wauzaji wa samaki na wajasiriamali wadogo katika soko hilo ambapo sasa mfumo huo unaweza kulipia kadri ya matumizi (PAYG), unaowawezesha wauzaji kulipia gesi wanayotumia tu na hivyo kuondoa gharama kubwa za kujaza mitungi na kupunguza matumizi ya kila siku hadi Shilingi 45,000.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataita Ferry jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 21, 2025 katika soko hilo Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment