Ads

WANANCHI WAALIKWA BANDA LA WANYAMA TAWA,LIPO SABASABA,MAGANJA AWEKA WAZI KILAKITU.

 

Afisa Habari wa MAMLAKA ya Wanyamapori Tanzania(TAWA) Beatusi Maganja amewataka wanchi kutembelea Banda la TAWA katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Maganja ametoa wito huo leo Julai 3,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la TAWA akiwaomba kutumia fursa ya maonesho kwenda kutembele na kujionea wanyama pori ambao wapo kabla ya kilele.

"Njooni watanzania kujionea wanyama kwani baadhi wanawaona wanyama katika kupitia luninga na kwenye mitandao ya kijamii lakini Leo hii ni fursa kuwaona wanyama pori kwa ukaribu zaidi na kwa uhuru",amesema Maganja Hata hivyo amesema katika maonesho haya ni fursa mojawapo kwa wananchi kwani unaweza kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na tabia za wanyama wakali na waharibifu kwa mfano fisi madoa unaweza kujifinza tabia zao na kujua namna gani yakuweza kuepuka hawa wanyama katika maeneo mbalimbali waliokokua wakisumbua.


Naye Mlezi wa Kituo kulelea watoto wenye mahitaji maalum na wanaoishi katika mazingira magumu cha Wezesha Kupaa YWAM Mwandege,Rebecca amefurahia kutembelea Banda la TAWA kwa kujionea wanyama mbalimbali ambapo watoto wamejionea kwa macho na kwamba walikua wanasoma darasani kwa kuona kwenye picha.

No comments